top of page

Uzazi wa Mpango 101: Njia za Kudumu

Uzazi wa Mpango 101

Tunafahamu kwamba kuchagua njia sahihi ya uzazi wa mpango kunaweza kuwa kugumu. Sio tu kuna njia nyingi za kuzichagua, lakini zote zinatekeleza kitu hicho hicho — kupunguza hatari ya ujauzito — katika njia tofauti tofauti sana! Nivi iko hapa kukusaidia ujifunze kuhusu njia mbalimbali zinazopatikana kwa ajili yako, na kuchagua moja inayokufaa wewe, mwenzi wako, na mtindo wako wa maisha. Ndio maana tumetengeneza mfululizo wa machapisho ya blogu kuhusu aina tofauti za njia za uzazi wa mpango na wakati gani zinatumika: papo hapo, muda mfupi, muda mrefu, kudumu, na za asili.


Hivyo, uko tayari kuona ni njia gani zilizopo? Endelea kuangazia!Njia za Kudumu

Hebu tulitazame hili. Muda mwingine, unajuwa tu hauhitaji watoto. Labda wazo la kuwa na watoto limekufanya kuwa na wasiwasi muda wote. Labda tayari una watoto zaidi kuliko unavyoweza kustahimili. Au labda mtoa huduma wako wa afya amekwambia kwamba wewe au mwenzi wako, hasa, hawezi kubeba mtoto mwenye afya hadi ujauzito utimize muda au kujifungua kwa usalama. Iwe sababu yoyote ile, unajua tu: kuwa na watoto ni kitu kigumu kutokea kwako. Vizuri, hiyo ni SAWA. Kiukweli kuna njia salama kabisa, za kiafya kwa ujumla kwa ajili yako na/au mwenzi wako kuwa na uhakika 100% kwamba hamuwezi kuwa na watoto wowote (au tena).


Utasishaji wa Mwanamke

(PIA INAJULIKANA KAMA Kufunga Mirija ya Mwanamke)


Wanawake ambao wanataka kuzuia ujauzito moja kwa moja wanaweza kufanyiwa kitu kinachoitwa “kufunga mirija.” Huu ni upasuaji wa kitabibu ambapo mirija ya uzazi ya mwanamke inafungwa, inakatwa, au kuzibwa (ndio maana kufunga mirija muda mwingine kunajulikana kama “kuifanya mirija yako ifungwe”). Mirija ya uzazi ni njia ambazo zinaunganisha mayai ya mwanamke na mfuko wake wa uzazi; bila mirija hiyo, sio tu mbegu ya kiume haitaweza kuyafikia mayai ya mwanamke, lakini pia mayai ya mwanamke hayataweza kuufikia mfuko wa uzazi na “kujishikilia” hapo—kitu ambacho kinahitajika kwa ajili ya mtoto kukua.


Faida:

 • Hupunguza hatari ya saratani ya mayai ya mwanamke

 • Ni fanisi sana kwenye kuzuia ujauzito (zaidi ya 99%!)

 • Huzuia ujauzito moja kwa moja; hakuna njia nyingine zitakazohitajika

 • Hufanyika papo hapo kwa wepesi na urahisi baada ya kujifungua kwa njia ya kawaida au kwa njia ya upasuaji, pindi tayari mwanamke yupo kliniki au hospitali; hivyo wanawake ambao hawataki tena watoto wanaweza kupanga kufunga mirija ya uzazi kabla (wakati wajawazito), au kuwaomba watoa huduma wao wa afya kuwafunga mirija ya uzazi wakati wa kujifungua


Hasara:

 • Sio salama, rahisi, au nafuu kama utasishaji wa mwanaume

 • Haikingi dhidi ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa (STIs)

 • Kwa sababu ni ya kudumu, mirija ya uzazi haiwezi kufunguliwa tena; wanawake lazima wawe na uhakika kuwa kamwe hawahitaji mtoto (au watoto zaidi) kabla ya kufanyiwa upasuaji huu


Utasishaji wa Mwanaume
(PIA INAJULIKANA KAMA Kufunga Mirija ya Mwanaume)

Kufunga mirija ya mwanaume ni aina ya uzazi wa mpango kwa mwanaume. Ni upasuaji wa kitabibu wa haraka, salama, na rahisi ambao hukata au huziba mrija unaounganisha korodani, au “mapumbu” ya mwanaume (yanayofahamika sana sana zaidi kama kende, kokwa, au golori, miongoni mwa majina mengine) kwenye uume wake. Kwa sababu korodani ndio mahali mbegu ya kiume ya mwanaume inatengenezwa (seli ndogo sana, zisizoonekana kwa macho ambazo uhitajika kuzalisha), hii inamaanisha kuwa pindi mwanaume anapomaliza “kumwaga” au “kupiga bao” wakati wa au baada ya uamshwaji au usisimkaji wa kimapenzi shahawa zake hazitakuwa na mbegu ya kiume. Mbegu ya kiume ni kiungo cha lazima kwenye kutengeneza mtoto—hivyo mwanaume ambaye alishwahi kufanyiwa upasuaji wa kufunga mirija ya kiume hatoweza kumpa mwanamke ujauzito!


Faida:

 • Ni salama, rahisi, na nafuu zaidi kuliko utasishaji wa mwanamke

 • Haina maumivu (kabla ya “ukataji” haujaanza eneo huwekewa ganzi)

 • Ni ya haraka sana, na wanaume wanaofanyiwa wanaweza kwenda nyumbani siku hiyo hiyo.

 • Ni fanisi sana kwenye kuzuia ujauzito (zaidi ya 99%!)


Hasara:

 • Haikingi dhidi ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa (STIs)

 • Kwa sababu ni ya kudumu, wanaume wanatakiwa kuwa na uhakika kuwa hawataki watoto (au watoto zaidi) kabla ya kufanyiwa upasuaji huu.

 • Matokeo sio ya papo hapo; baada ya kufunga mirija ya kiume, mwanaume anatakiwa kutumia aina nyingine ya uzazi wa mpango mpaka daktari au mtaalam wa huduma za afya atakapoweza kuthibitisha kuwa hakuna mbegu za kiume katika shahawa zake. Hii inaweza kuchukua miezi kadhaa, na pia uhitaji mwanaume amwage (apige bao) mara 15-20 kabla ya ngono isio salama (hii inapaswa “kusafisha” mbegu zozote za kiume zilizobakia kwenye mfumo wa mwanaume kabla ya kufunga mirija ya kiume).


 

Unataka kujifunza njia gani ni sahihi kwako, na wapi pa kuipata? Una maswali mengine kuhusu kujamiiana, ujauzito, maambukizi ya magonjwa ya zinaa yaani STIs, au uzazi wa mpango? Kumbuka unaweza kuchati na Nivi kwenye WhatsApp na Facebook Messenger muda wowote. Ni mazungumzo binafsi, ya usiri, na bure!


Comments


bottom of page