top of page

Uzazi wa Mpango 101: Njia za Asili

Uzazi wa Mpango 101

Tunajua kwamba kuchagua njia sahihi ya uzazi wa mpango kunaweza kuwa kugumu. Sio tu kuna njia nyingi sana za kuchagua, lakini zote zinafanikisha kitu kimoja — kupunguza hatari ya kupata ujauzito — katika njia nyingi tofauti! Nivi iko hapa kukusaidia ujifunze kuhusu njia mbalimbali zinazopatikana kwa ajili yako, na kuchagua moja ambayo inakufaa wewe, mpenzi wako, na mtindo wako wa maisha. Ndio maana tumetengeneza mfululizo wa machapisho ya blogu kuhusu aina tofauti tofauti za njia za uzazi wa mpango na ni wakati gani zinatumika: papo kwa hapo, muda mfupi, muda mrefu, za kudumu na za asili.


Hivyo, uko tayari kuona ni njia gani zilizopo? Endelea kuangaza!



Njia za Asili

Labda aina nyingine za njia za uzazi wa mpango zinakuogopesha. Labda usingetaka mtu yoyote afahamu kuwa unajaribu kuzuia ujauzito. Labda hauna tu uwezo wa kuzipata njia zingine tunazoziongelea. Haijalishi sababu yako ni ipi: ni sawa. Kuna njia za kuzuia ujauzito usiohitajika bila njia za kisasa, za kitabibu. Sio fanisi kiasi kile, lakini zitapunguza hatari yako ya kupata ujauzito.


Njia ya Kumwagia Nje (AKA Njia ya Kukojolea Nje)

Kati ya njia zote za asili, njia ya kumwagia nje ndio rahisi zaidi. Maana yake ipo kwenye jina! Inaitwa njia ya “kumwagia” nje kwa sababu hivyo ndivyo mwanaume hufanya wakati wa kujamiiana—huchomoa kumwagia nje, au kukojolea nje ya uke wa mwanamke kabla hajafika kileleni. Katika maneno mengine, mwanaume “humalizia” popote lakini si ndani yako. Hiyo inaweza kumaanisha juu yako, juu ya mashuka, au katika kitambaa—haijalishi, ili mradi sio sehemu ilio karibu na sehemu zako za siri!


Faida:

  • Kama njia nyingine za asili, ni yenye faida wakati hauwezi kutumia njia za kisasa, za kitabibu kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa mpenzi au familia yako, au kwa sababu ni ngumu kwenda kliniki au kwa mtoa huduma za afya

  • Ni nyepesi kuielewa na rahisi zaidi kuliko njia nyingine za asili

  • Inaweza kufanyika muda wowote—iwe unatumia njia nyingine ya uzazi wa mpango au hautumii


Hasara:

  • Muda mwingine uhitaji kujisafisha baada ya tendo

  • Uhitaji kumuamini SANA mpenzi wako (mpenzi wa kiume ndio mtekelezaji mkuu)

  • Kwa sababu mbegu za kiume zinaweza kutolewa kutoka kwenye uume wakati wa kujamiiana na pia wakati ukiwa kileleni, bado ni hatari; na sio fanisi kama njia za kisasa, za kitabibu

  • Haimlindi yoyote kati ya wapenzi wawili dhidi ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa (STIs)


Njia ya Mzunguko wa Hedhi (AKA Njia ya Kalenda)

Kama wewe ni mwanamke na unapata hedhi za mara kwa mara, kuna siku chache kila mwezi ambapo una uwezekano mdogo wa kupata ujauzito. Njia ya mzunguko wa hedhi, pia ijulikanayo kama njia ya kalenda, hutumika siku hizo kwa kuhamasisha kujamiiana TU kipindi hicho, na si wakati mwingine wa mwezi. Ni sahihi—unatengeneza ratiba kwa ajili ya kujamiiana! Kama siku ya 1 ndio siku hedhi yako inapoanza, basi njia ya mzunguko wa hedhi husema unaweza kujamiiana kwenye siku ya 1-7 na ya 20 kuendelea (ambapo unakuwa na uwezo mdogo wa kushika ujauzito na hivyo kuwa na uwezo mdogo wa kuwa mjamzito), na unaepuka kujamiiana kwenye siku ya 8 hadi ya 19 (ambapo una uwezo mkubwa wa kushika ujauzito).


Faida:

  • Kama njia nyingine za asili, ni yenye faida wakati hauwezi kutumia njia za kisasa, za kitabibu kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa mpenzi au familia yako, au kwa sababu ni ngumu kwenda kliniki au kwa mtoa huduma za afya

  • Inaweza kufanyika muda wowote—iwe unatumia njia nyingine ya uzazi wa mpango au hautumii


Hasara:

  • Kila mwanamke yuko tofauti! Ikimaanisha mzunguko wa hedhi wa kila mwanamke uko tofauti, na siku za kushika ujauzito za kila mwanamke ziko tofauti. Hivyo kwa sababu tu mwanamke mmoja hana uwezo wa kupata ujauzito kwenye siku ya 8 hadi ya 19 haimaanishi hauna uwezo wa kupata ujauzito kwenye siku ya 8 hadi ya 19

  • Ina hatari ya kutokukuepusha na ujauzito, na sio fanisi kama njia za kisasa, za kitabibu

  • Haimlindi yoyote kati ya wapenzi wawili dhidi ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa (STIs)


Kutokupata hedhi wakati wa kunyonyesha (AKA njia ya kunyonyesha)

Wanawake ambao wamejifungua katika miezi 6 iliyopita na wamekuwa wakinyonyesha tangu walipojifungua—walau masaa 4 kila mchana na masaa 6 kila usiku—na hawatumii kitu chochote mbali na kunyonyesha kuwalisha watoto wao, hawapevushi mayai.

Upevushaji yai ni wakati mfuko wa mayai unapotoa yai ili liweze kurutubishwa na mbegu ya mwanaume; hivyo, kama mwanamke hapevushi mayai, inamaanisha hawezi kupata ujauzito. Ni muhimu kujua kuwa mwanamke ambaye hapevushi mayai pia hatopata hedhi. Hivyo, kama unapata hedhi baada ya kujifungua, hata kama unatokwa damu siku chache tu kama siku mbili, inawezekana pia unapevusha mayai (na hivyo unaweza kupata ujauzito)


Faida:

  • Pindi ikifanyika kikamilifu kabisa, njia hii inaweza kuwa fanisi kukaribia njia za kisasa, za kitabibu

  • Ni rahisi sana kuifanya (“Umejifungua? Nyonyesha tu sana!”)

  • Kama njia nyingine za asili, ni yenye faida wakati hauwezi kutumia njia za kisasa, za kitabibu kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa mpenzi au familia yako, au kwa sababu ni ngumu kwenda kliniki au kwa mtoa huduma za afya

  • Inaweza kufanyika muda wowote—iwe unatumia njia nyingine ya uzazi wa mpango au hautumii


Hasara:

  • Inaweza kutumika tu kwa miezi 6 ya kwanza ya maisha ya mtoto mpya

  • Wanawake wanaweza kuwa wajawazito hata mwezi 1 baada ya kujifungua, iwe wanatumia njia hii au hawatumii!

  • Inahitaji kunyonyesha sana—kitu ambacho sio wanawake wote wana uwezo wa kukifanya (kwa sababu hawatengenezi maziwa ya kutosha, watoto wao wana shida kwenye kukamata chuchu ili wanyonye, au wana kazi au majukumu ya nyumbani ambayo yanawakwamisha kunyonyesha mara nyingi kadri wanavyohitajika)

  • Wanawake ambao huwapa watoto wao maziwa ya fomula (hata kama wananyonyesha pia) hawawezi kutumia njia hii kama njia ya uzazi wa mpango ya kutegemea

  • Ina hatari ya kutokukuepusha na ujauzito, na sio fanisi kama njia za kisasa, za kitabibu

  • Haimlindi yoyote kati ya wapenzi wawili dhidi ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa (STIs)


 

Unataka kujifunza njia ipi ni sahihi kwako, na wapi pa kuipata? Una maswali mengine kuhusu kujamiiana, maambukizi ya magonjwa ya zinaa yaani STIs, na uzazi wa mpango? Kumbuka unaweza kuchati na Nivi kwenye WhatsApp na Facebook Messenger muda wowote. Ni mazungumzo binafsi, ya usiri, na bure!

Comments


bottom of page