top of page

Ujauzito wa Nje ya Mfuko wa Uzazi

Ujauzito wa nje ya mfuko wa uzazi ni sababu inayoongoza ya vifo vya kina mama wajawazito katika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito na huchangia vifo vya kina mama wajawazito kwa walau 10%. Ili kujua ni kwanini, hebu tutazame tofauti kati ya ujauzito wa kawaida na ujauzito wa nje ya mfuko wa uzazi. Tutahitaji kwanza kupitia sehemu baadhi muhimu za mfumo wa uzazi wa mwanamke:

  • Yai ni seli ya uzazi ya mwanamke ambayo imepevuka. Yakiwa mengi huitwa mayai.

  • Vifuko viwili vidogo vinavyoitwa mifuko ya mayai hutengeneza vichocheo vya mwanamke vya uzazi na mayai.

  • Mirija ya uzazi huunganisha mifuko ya mayai kwenye mfuko wa uzazi pande zote mbili. Hii ndio njia yanapopitia mayai kutoka kwenye mifuko ya mayai kwenda kwenye mfuko wa uzazi.

  • Kiini ni yai ambalo limerutubishwa na mbegu ya kiume.

  • Mfuko wa uzazi ni jina lingine la tumbo la uzazi. Ujauzito hutokea pindi kiini kilichorutubishwa kinapojipandikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi.

Kama unavyojua, mifuko ya mayai hutoa yai kwenda kwenye mirija ya uzazi wakati wa upevukaji wa yai. Kama yai likirutubishwa na mbegu ya kiume wakati linapokwenda kwenye mfuko wa uzazi, litahitaji sehemu fulani ili likue. Katika ujauzito wa kawaida, kiini kilichorutubishwa kitajipandikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi na kukua kuwa mtoto. Mfuko wa uzazi una kuta imara zenye misuli ambazo zinaweza kuvutika, kitu ambacho humpa mtoto nafasi ya kutosha kukua.



Ujauzito wa Nje ya Mfuko wa Uzazi ni Nini?

Katika ujauzito wa nje ya mfuko wa uzazi, kiini kilichorutubishwa hukua nje ya mfuko wa uzazi. Katika kesi nyingi, kiini kilichorutubishwa hukwama ndani ya mirija ya uzazi kikiwa njiani kuelekea kwenye mfuko wa uzazi na kuanza kukua hapo. Hali hii ni ya hatari kwa sababu mirija ya uzazi haijatengenezwa kubeba mtoto anayekua kama ulivyo mfuko wa uzazi. Matokeo yake, mrija wa uzazi utachanika ikiwa kiini kilichorutubishwa kitaendelea kukua kikiwa hapo kitu ambacho kinaweza kupelekea uvujaji damu wa ndani kwa ndani na kifo cha mama mjamzito.



Vya Muhimu

  1. Kiini kilichorutubishwa

  2. Mfuko wa uzazi

  3. Mrija wa uzazi

Mchoro wa ujauzito wa kawaida (kushoto) unaonesha kiini kilichorutubishwa kilichojipandikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi ambapo kinapaswa kukua kikiwa hapo. Mchoro wa ujauzito wa nje ya mfuko wa uzazi (kulia) unaonesha kiini kilichorutubishwa kilichojipandikiza kwenye mrija wa uzazi. Mrija wa uzazi utachanika ikiwa kiini kilichorutubishwa kitaendelea kukua hapo kitu ambacho kinaweza kupelekea uvujaji wa damu ndani kwa ndani na kifo cha mama mjamzito.



Ninajua Vipi Kama Nina Ujauzito wa Nje ya Mfuko wa Uzazi?

Ujauzito wa nje ya mfuko wa uzazi una dalili sawa za mapema za ujauzito wa kawaida kama vile kutokuona hedhi, maumivu ya matiti, na kichefuchefu. Hata hivyo, kuna dalili fulani za msingi za ujauzito wa nje ya mfuko wa uzazi za kuziangalia. Utokaji damu mwepesi kwenye uke na maumivu ya nyonga kwa kawaida ndio dalili za kwanza za hatari kutokea. Ikiwa dalili hizi zinaambatana na hali ya wepesi wa kichwa, kuzimia, maumivu ya bega, au maumivu ya tumbo, tafadhali nenda hospitali moja kwa moja.



Sababu za hatari ni nini?

Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza

kuongeza hatari yako ya kupata ujauzito wa nje ya mfuko wa uzazi, kama vile:

Wakati hauwezi kuzuia ujauzito wa nje ya mfuko wa uzazi, kuna vitu baadhi unavyoweza kufanya kupunguza hatari yako:

  • Kutumia kondomu wakati wa kujamiiana kunaweza kuzuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa yaani STI’s na kunaweza kupunguza hatari ya maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke yaani PID

  • Usivute sigara, hasa kama unapanga kuwa mjamzito



Matibabu ni nini?

Kwa bahati mbaya, ujauzito wa nje ya mfuko wa uzazi hauwezi kuendelea hadi kuzaliwa kwa mtoto kwa sababu kiini kilichorutubishwa hakiwezi kukua nje ya mfuko wa uzazi. Kwa nyongeza, inaweza kuwa hatari sana kwa mama ikiwa mrija wa uzazi utachanika. Hivyo, matibabu ya kawaida ni kukiondoa kiini kilichorutubishwa ili kuzuia masuala makubwa ya kiafya. Hii inaweza kufanyika kwa njia mbili. Chaguo la kwanza ni kutumia dawa ambayo husimamisha ukuaji wa kiini kilichorutubishwa na kukatisha ujauzito. Chaguo la pili ni kukiondoa kwa upasuaji. Kutafuta matibabu haraka iwezekanavyo kunaweza kuokoa maisha ya mama.



 

Una maswali mengine kuhusu kujamiiana, Maambukizi ya magonjwa wa zinaa yaani STIs, na uzazi wa mpango? Kumbuka unaweza kuchati na Nivi kwenye WhatsApp na Facebook Messenger muda wowote. Ni mazungumzo binafsi, ya usiri, na bure!






Comments


bottom of page