top of page

Ugonjwa wa Kabla ya Hedhi: Ukweli na Uzushi

Ugonjwa wa Kabla ya Hedhi, kwa kitaalamu, Premenstrual Syndrome (PMS) ni kundi la dalili ambazo humtokea mwanamke kabla au wakati wa hedhi yake. Dalili hubadilika kutoka ukasirikaji na sonona hadi uchu wa chakula na kitu chochote kitakachotokea katikati ya hivyo. Mara nyingi, ishara na dalili za PMS zinaweza kuchukuliwa kama mwanamke ‘ana hisia kali’. Kiukweli, watu huenda mbali hata kuisema PMS kama ni kitu cha kweli. Hayo yakiwa yamesemwa, Nivi iko hapa kuukabili uongo na kuuthibitisha ukweli!


1) PMS iko kichwani mwako.


UZUSHI: PMS ni jambo la kweli. Muunganiko wa baadhi ya au dalili zote kama ukasirikaji, kuchoka, wasiwasi, na hisia za huzuni zote zinaweza kuwa sababu za PMS kabla au wakati wa hedhi yako. PMS inaweza kutokana na ubadilikaji wa viwango vya homoni kwa sababu viwango vya homoni za mwili wako hujirekebisha pindi mwili wako ukigundua wewe si mjamzito. Hivyo, muda ujao ukikasirishwa na kile kinachoonekana kama sababu isio na mashiko, fahamu kuwa hisia zako ni sahihi na mwishowe zitapita!


2) Kuna madini na vitamini fulani za kutumia kusaidia kufifisha dalili za PMS

UKWELI: Kalsiamu na Vitamini C zimethibitishwa kusaidia kufifisha dalili za PMS kama maumivu ya tumbo, ukasirikaji, tumbo kujaa, wasiwasi na kuchoka. Unaweza kuipata Kalsiamu na Vitamini C katika virutubisho, lakini kama ungependelea kuviunganisha katika mlo wako jaribu vyakula kama maziwa, jibini, na yogati kwa ajili ya Kalsiamu, na matunda jamii ya machungwa, mboga za majani za kijani, na viazi vyeupe kwa ajili ya Vitamini C!


3) PMS humuathiri kila mtu anayepata hedhi.


UZUSHI: Ikiwa hupati dalili zozote za PMS ni sawa kabisa, kiukweli, unapaswa kujichukulia mwenye bahati! Si wanawake wote hupata hii, lakini ni wazi haimaanishi wanawake ambao hupata wanapaswa kudharauliwa.


4) Hisia na dalili zangu ni sahihi licha ya nini mtu yoyote anasema!


UKWELI: Haijalishi nini mtu yoyote anasema ambacho kinajaribu kuchukulia kiuwepesi hisia zako au kupuuza dalili zako, fahamu kuwa kile unachokihisi ni kweli na sahihi! Licha ya uzushi ambao watu wanaweza kusema kuhusu PMS kuwa si kitu cha ‘kweli’, kuna ushuhuda mwingi ambao unathibitisha kinyume chake. Kumbuka tu kuichukulia kawaida, jaribu kula Kalsiamu na Vitamini C nyingi na pata mapumziko. Dalili zitakwisha ndani ya muda mfupi.


Unataka kujifunza zaidi? Una maswali mengine kuhusu kujamiiana, maambukizi ya magonjwa ya zinaa yaani STIs, UKIMWI, au uzazi wa mpango? Kumbuka unaweza kuchati na Nivi kwenye WhatsApp na Facebook Messenger muda wowote. Ni mazungumzo binafsi, ya usiri, na bure!Comments


bottom of page