Siku ya furaha kwa kina mama!
Nawatakia heri siku hii ya kina Mama kwa nyinyi wakina mama wote! Mwaka huu, tulifikiri itakuwa raha kuzungumza juu ya hekima ya mama-kwa sababu kawaida, kina mama ndio watu wenye busara zaidi tunaowajua! Je, ni ushauri gani bora mama yako amekupa? Tuliuliza wenzetu hapa Nivi, na tukashirikiana ushauri mama zetu waliotupatia kwa miaka zilizopita. Chini ni chache ambazo zilionekana sana:
La kufurahisha zaidi
"Usioge wakati wa mvua ya ngurumo."
Ya Vitendo Zaidi
"Osha vyombo kadri unavyovitumia ili visirundike."
Mzuri zaidi
"Tunza familia yako."
Inayohamasisha zaidi
"Usikate tamaa. Kuwa hodari kukabiliana na hali yoyote ile. ”
Ya Kiroho Zaidi
"Chukua muda katika siku yako ili kuomba na kutafakari."
Ya Kutuhumu zaidi
"Bei inajadiliwa kila wakati."
Na wewe je? Je, ni ushauri gani mama yako alikupa ambayo unakumbuka hadi wa leo? Je, ilikuwa na manufaa? Inachekesha? Inachochea? Tujulishe, kwa kutoa maoni hapa chini, au kwenye Instagram yetu!
Na kwa ushauri ambao huwezi kumuuliza mama yako, muulize Nivi! askNivi inapatikana kukupa ushauri wa kiafya na habari 24/7 kwenye Facebook Messenger na WhatsApp.
Comments