top of page

Mwezi wa Kuhamasisha Uelewa wa Afya ya Shingo ya Kizazi!



Ni Januari, ikimaanisha ni Mwezi wa Kuhamasisha Uelewa wa Afya ya Shingo ya Kizazi! Kujifunza na kusambaza elimu juu ya afya ya shingo ya kizazi ni muhimu sana kwa sababu kama isipofuatiliwa vizuri inaweza kuathiri idadi kubwa ya watu kutoka jamii zote. Habari njema, hata hivyo, ni kuwa saratani ya shingo ya kizazi ni moja ya aina za saratani zinazoepukika na kutibika kabisa. Kuna njia zaidi kuliko moja ambazo askNivi inaweza kuhakikisha hauachwi nyuma unapochukua tahadhari za kujiepusha dhidi ya virusi vinavyosababisha saratani ya shingo ya kizazi yaani HPV na saratani ya shingo ya kizazi.


Pata Chanjo!


Kulingana na CDC, kupata chanjo dhidi ya HPV hulinda watu dhidi ya aina za HPV ambazo mara nyingi ndio sababu ya saratani za shingo ya kizazi, uke na via vya uzazi vya mwanamke. Upataji chanjo ni muhimu hasa kwa mabinti wadogo, wenye umri wa miaka 11 na 12, au kama umri huo umepita, kwa kila mwanamke mwenye hadi umri wa miaka 26. Kama una miaka zaidi ya 26, basi chanjo hii inaweza isiwe chaguo bora na ni muhimu kuongea na mtaalamu wa afya. Kwa bahati nzuri, AskNivi inaweza kukuunganisha na kliniki iliyo karibu zaidi kupata au kujadili juu ya chanjo!




Vipimo vya Uchunguzi:

Pamoja na kupata chanjo dhidi ya HPV, pia kuna vipimo viwili ambavyo vinaweza kusaidia kuepusha saratani ya shingo ya kizazi. Kipimo cha Pap na/au kipimo cha HPV.

  • Kipimo cha Pap: huangalia viashiria vya saratani ambavyo vingeweza kuwa saratani ya shingo ya kizazi kama visingetibiwa au kuangaliwa kwa uangalifu. Wanawake wanapaswa kuanza kupata kipimo cha pap kwenye umri wa miaka 21. Kati ya umri wa miaka 21-29, kama seli zinaonekana ni za kawaida, kipimo hiki kinapaswa kufanyika kila baada ya miaka 3 na kutoka umri wa miaka 30-65 kinapaswa kufanyika kila baada ya miaka 5.

  • Vipimo vya HPV: vinapaswa kufanyika kwa wanawake wenye umri wa miaka 21-29 TU kama majibu ya kipimo cha pap yanaonesha utata. Wanawake wenye umri wa miaka 30-65 wanapaswa kufanya kipimo cha HPV kila baada ya miaka 5 bila kujali kitu chochote.

Haya yanaweza kuonekana kama maelezo mengi, lakini usiwe na wasiwasi, askNivi iko hapa kukusaidia! Asknivi inaweza kukuunganisha na kliniki yako ya karibu zaidi ili kwamba uweze kuanza kupata vipimo vyako kujihakikishia maisha ya furaha na yenye afya.

Mabadiliko ya Mtindo wa Maisha

Tuyaweke mahudhurio ya kliniki pembeni, kuna machaguo fulani ya mtindo wa maisha ambayo pia yanaweza kusaidia kuepusha uwezekano wako wa kupata saratani ya shingo ya kizazi. Njia za kujiepusha tatu muhimu zinahusisha, kuacha kuvuta sigara, kutumia kondomu wakati wa kujamiiana, na kutokuwa na wapenzi wengi.


Kwa kufuata hatua hizi utakuwa unaifahamu afya yako ya shingo ya kizazi na kusaidia kupunguza hatari za HPV!


Unataka kujifunza zaidi? Una maswali mengine kuhusu kujamiiana, STIs, HIV/AIDS, au uzazi wa mpango? Kumbuka unaweza kuchati na Nivi kwenye WhatsApp na Facebook Messenger muda wowote. Ni kwa faragha, kwa usiri, na bure!


Comments


bottom of page