top of page

Maumbile, Jinsia na Ujinsia Vimeelezewa

Maumbile, jinsia na ujinsia ni sehemu za utambulisho wetu wa kila siku. Kuelewa nini kinachukuliwa ni umbile, jinsia, au ujinsia ni kipengele muhimu cha jamii. Kufahamu ni nini vinamaanisha, na maneno ambayo yanayodondokea chini ya kila kundi, kunaweza kusaidia kukuza hisia ya jamii ambayo ni jumuishi na kuelewana kwa mmoja na mwingine. Makala hii itachanganua maana ya kila kundi, na pia kuelezea utambulisho ambao unadondoka chini ya kila kundi kati ya makundi hayo matatu.


Maneno “jinsia”, “umbile”, na “ujinsia” yameteka vyombo vya habari katika miaka ya karibuni. Watu wanayajadili mara kwa mara na kwa wazi zaidi kwenye mitandao ya kijamii, vile vile na marafiki na familia. Lakini hata kama kujadili mada hizi kunakuwa ni kawaida na kunakubalika zaidi kijamii, maana zake za kweli zinaweza kupotezwa na kuharibiwa katika mchakato huo. Ndio maana tulifikiri mchanganuo ungekuwa wa muhimu—maelezo ya maneno yote haya na nini yanamaanisha, kukusaidia kuelewa masuala haya vizuri zaidi na kukuandaa kwa ajili ya mazungumzo yasiotarajiwa na wapendwa wako. Hivyo, hebu tuanze!


Je! Kwanini jinsia, maumbile, na ujinsia ni vya muhimu sana?


Jinsia, maumbile, na ujinsia ni sehemu ya sisi ni kina nani, aidha tunalitambua hilo au la. Sote kati yetu tuna jinsia, umbile, na ujinsia—ni vile tu hatuvifikirii mara kwa mara. Haswa pindi jinsia na maumbile yetu yanaporandana, au pindi jinsia zetu ziko wazi kwa watu wanaotuzunguka kwasababu ya namna tunavyoonekana. Kwa wengine, hata hivyo, haiko moja kwa moja sana.


Zaidi ya hayo, ujinsia ni sifa iliyofichika; haiko wazi kwa kumuangalia tu mtu. Na kwa wengi, kutambua ujinsia wao kunachanganya sana, au ni ngumu zaidi. Wao pia ni sehemu muhimu ya jamii tunayoishi. Hivyo kujua maneno haya yanamaanisha nini, na maneno ambayo yanadondokea chini ya kila kundi, sio tu inaweza kutusaidia kujielewa sisi wenyewe vizuri zaidi, lakini pia kukuza hisia ya jamii ambapo kuelewa na kukubali ni kawaida, na sio upuuzaji.Umbile ni mionekano ya mtu kimwili, haswa aliyopewa kwenye kuzaliwa. Umbile analopewa mtu linaitwa ‘umbile la kuzaliwa’ na linachanganuliwa katika machaguo matatu:


 • Wa kiume → mwanaume au mvulana ambaye hasa ana uwezo wa kuzalisha mbegu za kiume kutokana na muonekano wa kuwa na uume na korodani


 • Wa kike → mwanamke au msichana ambaye ana uwezo wa kuzalisha au kutoa mayai ya kike kutokana na muonekano wa kuwa na mfuko wa uzazi na uke


 • Mwenye Maumbile Mawili → mtu aliyezaliwa na tofauti mbalimbali katika sifa zake za kimaumbile ndani na nje ya mwili. Hii inaweza kuhusisha tofauti kati ya sehemu za siri, kromosomu, viungo vya uzazi vya ndani na zaidi!

Jinsia ni pana na inategemea juu ya jinsi mtu anavyochagua atambulike. Mtu anaweza kujitambulisha kwa jinsia ambayo ni sawia au tofauti na umbile lake alilopewa kwenye kuzaliwa. Tayari tumeshaelezea wa kiume, wa kike, na wenye maumbile mawili, lakini chini hapa ni tambulisho zaidi za jinsia na zinavyomaanisha:


 • Mtu aliyebadili jinsia → mtu ambaye utambulisho wake wa jinsia ni tofauti na umbile alilopewa kwenye kuzaliwa. Watu baadhi wanaweza kuzifanyia upasuaji sehemu maalum za mwili ili sifa zao za kimwili ziendane na jinsi wanavyohisi ndani.


 • Mwenye jinsia mbili → mtu ambaye hawezi kujitambulisha kama wa kiume tu au wa kike tu. Watu wenye jinsia mbili wanaweza kujitambulisha kama mwanaume na mwanamke kwa pamoja, kama nje ya makundi haya, au mahali fulani katikati!


 • Anayebadilika jinsia → Watu ambao hujitambulisha kama wanaobadilika jinsia haswa hukataa makundi ya wenye jinsia mbili na kupenda ubadilikaji wa jinsia, kama jinsi tu tulivyojadili jinsia kuwa ni pana. Watu wanaobadilika jinsia wanaweza kujiona kama ni wa kiume na wa kike kwa pamoja, wako nje ya kundi, au sio wa kiume au wa kike


 • Asiyekuwa na jinsia → mtu ambaye hatambuliki kuwa na jinsia yoyote maalum


 • Mwenye jinsia iendanayo na umbile → neno linalotumika kumuelezea mtu ambaye jinsia yake inarandana na umbile lake kwenye kuzaliwa. Idadi kubwa ya watu hupenda kujitambulisha kama wenye jinsia ziendanazo na maumbile.


 • Mwenye jinsia inayobadilika → mtu ambaye jinsia yake inabadilika/kuendana na hali mara nyingi – mtu ambaye hajitambulishi kuwa na jinsia fulani tuUjinsia unahusiana na utambulisho wa jinsia ya mtu kwasababu unahusiana na jinsia gani au jinsia zipi ambazo mtu huyo anavutiwa nazo haswa. Kama tu jinsia, ujinsia pia ni mpana wenye utambulisho tofauti tofauti. Chini hapa ni utambulisho kadhaa wa ujinsia na maelezo yao:


 • Shoga → Mtu ambaye anavutiwa na mtu mwingine wa jinsia sawa aidha kihisia, kimapenzi, na/au kingono. Neno ‘shoga’ huwaelezea wanaume wanaovutiwa na wanaume, lakini pia linatumika kama neno la ujumla linaloelezea mtu yoyote anayevutiwa na mtu mwingine wa jinsia sawa.


 • Msagaji → mwanamke ambaye anavutiwa na wanawake wengine kihisia, kimapenzi na/au kingono


 • Anayevutiwa na jinsia mbili → Mtu ambaye anavutiwa na jinsia zaidi ya moja kihisia, kimapenzi na/au kingono. Haswa hii huelezea mtu ambaye ana mvuto kwa mtu mwingine wa umbile sawa au umbile tofauti na la kwake


 • Asiyevutiwa kimapenzi → Mtu ambaye hana kabisa au anavutiwa kimapenzi kidogo au anayekosa shauku ya kufanya mapenzi na wengine. Kama kuwa na hisia za mapenzi, kutokuwa na hisia za mapenzi ni jambo pana, hivyo watu baadhi wanaweza wakawa na mvuto wa mapenzi kiasi, kidogo au wasiwe nao, lakini bado wanaweza wakawa na mvuto wa kufanya mapenzi.


 • Anayevutiwa na kila mtu → Mtu ambaye anavutiwa kingono, kimapenzi na/au kihisia na watu bila kujali maumbile na jinsia zao. Watu wanaovutiwa na kila mtu muda mwingine wanajielezea kama “wenye upofu wa jinsia” kwasababu jinsia na maumbile ya mtu sio sababu za kuamua mvuto wao kwa mtu huyo.


 • Anayebadilika jinsia → neno anayebadilika jinsia mara nyingi hutumika kuelezea aina mbalimbali za tambuzi na ujinsia ambazo huchangamana na jinsia na ujinsia kuu (m.f. mwanaume).

 • Anayevutiwa kihisia kwanza → huelezea mtu ambaye hupata mvuto wa kimapenzi kwa mtu BAADA ya kupata mvuto wa kihisia kwa mtu huyo. Mtu anayevutiwa kihisia kwanza anaweza kuwa shoga, anayevutiwa na jinsia mbili, anayevutiwa na kila mtu, n.k., lakini bado lazima apate mvuto wa kihisia kabla ufanyaji mapenzi haujatambulishwa katika uhusiano.

Kwa ujumla, maumbile, jinsia na ujinsia vyote ni vitu vya kusherehekewa! Yoyote uliye, unayempenda au unavyojitambulisha ni kitu cha kujivunia. Ikiwa hauna uhakika au haujisikii sawa na utambulisho wako, kumbuka kuwa vitu huchukua muda na hii ni safari kwa ajili yako mwenyewe kuigundua. Orodha hiyo juu yote ni alama tu, na ikiwa haujisikii sawa na alama basi hilo ni sawa, pia! Hata hivyo, chochote kile mtu fulani anachochagua kujitambulisha nacho kinapaswa kuheshimiwa kama namna ya kukuza mazingira jumuishi na salama.Unataka kujifunza zaidi? Una maswali mengine kuhusu kujamiiana, maambukizi ya magonjwa ya zinaa yaani STIs, UKIMWI, au uzazi wa mpango? Kumbuka unaweza kuchati na Nivi kwenye WhatsApp na Facebook Messenger muda wowote. Ni mazungumzo binafsi, ya usiri, na bure!


Comments


bottom of page