top of page

Maambukizi ya Yeast: Nini kinaendelea sehemu za siri?Ikiwa umewahi kuhisi muwasho sana “sehemu za siri” hiyo inaweza kuwa ishara kwamba una maambukizi ya yeast… lakini husiofu! Maambukizi ya yeast ni ya kawaida sana na yanatibika kwa urahisi. Hapa, tutaangazia yote unayohitaji kujuwa kuhusu maambukizi ya yeast: ni nini, jinsi ya kuyatibu, na nini unaweza kufanya kuyaepuka. Endelea kusoma kujifunza zaidi!


Maambukizi ya yeast ni nini?

Yeast (aina ya fangasi) waitwao Kandida kwa kawaida huishi ndani ya uke wako bila matatizo yoyote. Mara nyingine yeast huyu anaweza kuzaliana kupitiliza na kusababisha maambukizi ya yeast, yajulikanayo pia kama maambukizi ya kandida. Haya ni ya kawaida sana! Wanawake na wasichana wengi watapata maambukizi ya yeast ukeni wakati fulani katika maisha yao.


Zipi ni dalili?

Maambukizi ya yeast yanaweza kuwa ya kuudhi sana- husababisha kuwashwa, hali ya wekundu, au kukereketwa katika sehemu zako za siri. Maambukizi ya yeast yanaweza pia kusababisha ute mweupe mzito kwenye nguo yako ya ndani ambao unaonekana kama jibini. Dalili nyingine ni maumivu au kuungua wakati wa kukojoa au kujamiiana. Kama ukigundua yoyote kati ya dalili hizi, muone mhudumu wako wa afya kwa uchunguzi! Anaweza kusema kama ni maambukizi ya yeast na akapendekeza matibabu.


Maambukizi ya yeast yanatibiwaje?

Kuna njia nyingi za kutibu maambukizi ya yeast! Dawa za kumeza na krimu za fangasi zinaweza kuondoa dalili baada ya siku chache na kutibu maambukizi ndani ya wiki. Baadhi ya maambukizi ya yeast yanaweza kuisha yenyewe, lakini ni vizuri yachunguzwe na mhudumu wa afya. Chaguo lolote la matibabu utakalochagua, ni muhimu kutumia dawa kwa muda ambao mhudumu wako wa afya kakuelekeza; kuacha dawa mapema sana kunaweza kusababisha maambukizi ya yeast kurudi. Muone mhudumu wako wa afya kuangalia ni matibabu gani yanafanya kazi vizuri zaidi kwako!Maambukizi ya yeast yanaambukizwa kwa kujamiiana?

Habari njema ni hapana; maambukizi ya yeast si ugonjwa wa kuambukizwa kwa kujamiiana (STD). Hata hivyo, ngono isio salama inaweza kuingiza bakteria wapya ukeni mwako, ambao wanaweza kupelekea ukuaji wa kupitiliza wa yeast. Kutumia mipira na kondomu kunaweza kupunguza uwezekano wako wa kupata maambukizi ya yeast.


Baadhi ya magonjwa ya kuambukizwa kwa kujamiiana yaani STDs yanaweza kusababisha dalili sawa na maambukizi ya yeast, kama vile hali ya muwasho, hali ya wekundu, na kukereketwa katika sehemu zako za siri. Ndio maana ni muhimu kupimwa mara kwa mara magonjwa ya kuambukizwa kwa kujamiiana yaani STDs kwenye kliniki yako ya jirani!


Nina maambukizi ya yeast…ninaweza bado nikajamiiana?

Maambukizi ya yeast sio ugonjwa wa kuambukizwa kwa kujamiiana yaani STD, lakini hiki hapa ndicho unapaswa kuzingatia kabla ya kujamiiana. Kwanza, kujamiiana ukiwa na maambukizi ya yeast kunaweza kuwa kwenye maumivu na kwenye kuudhi. Pili, krimu inayotumika kutibu maambukizi ya yeast inaweza kusababisha kondomu kupasuka, kitu ambacho kinaweza kuongeza hatari yako ya kupata ujauzito au ugonjwa wa kuambukizwa kwa kujamiiana yaani STD. Kwa sababu hizi, ni vizuri zaidi kuepuka kujamiiana hadi maambukizi yako yatakapoisha.
Ninaweza kufanya nini kuepuka maambukizi ya yeast?

Yeast hupenda kukua katika maeneo ya joto, yenye unyevu hivyo epuka nguo zinazobana ambazo hutunza joto na unyevu. Kwa mfano, kuvaa nguo zinazopwaya na nguo ya ndani iliyotengenezwa kwa pamba kunaweza kusaidia kuziweka sehemu zako za siri katika hali ya ukavu.


Mara nyingine, sababu nyingine zinaweza kupelekea maambukizi ya yeast, kama vile:

  • Ujauzito

  • Vidonge vya uzazi wa mpango na njia nyingine za uzazi wa mpango zenye vichocheo

  • Mfumo wa kinga ulio dhaifu kwa sababu ya ugonjwa

  • Kutumia antibayotiki

  • Kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu au kisukari kisichotibiwa vizuri


Sababu hizi zinaweza kuwatibua bakteria “wazuri” ndani ya uke wako ambao huwazuia yeast wasikue kupitiliza. Ikiwa unafikiri yoyote kati ya sababu hizi zinaweza zikawa zinakusababishia maambukizi ya yeast, mjulishe mhudumu wako wa afya.


Kumbuka, Nivi iko hapa kukusaidia wewe na afya yako. Utakavyochunguzwa mapema zaidi na mhudumu wa afya, ndivyo utakavyoanza matibabu mapema zaidi na kujihisi vizuri zaidi!

 

Una maswali mengine kuhusu kujamiiana, magonjwa yanayoambukizwa kwa kujamiiana yaani STIs, na uzazi wa mpango? Kumbuka unaweza kuchati na Nivi kwenye WhatsApp na Facebook Messenger muda wowote. Ni mazungumzo binafsi, ya usiri, na bure!

Comments


bottom of page