Kukabiliana na Maumivu ya Hedhi: Dondoo, Mbinu, na Wakati Gani wa Kumuona Daktari
Oh hapana! Ni muda ule wa mwezi na una maumivu makali ya tumbo. Ni kawaida kuhisi maumivu chini ya tumbo lako, miguu, na mgongoni wakati wa hedhi yako. Habari njema ni kwamba kuna njia baadhi rahisi za kutuliza maumivu yako ya hedhi. Endelea kusoma kujifunza zaidi!
Hivyo kwanza, nini husababisha maumivu ya hedhi? Pindi ukiwa kwenye hedhi yako, mfuko wako wa uzazi hukaza na kulegea kusaidia kusukuma damu itoke nje ya uke. Mjongeo huu unaweza kusababisha maumivu makali ya tumbo kabla na wakati wa hedhi yako.

Maumivu ya hedhi ni ya kawaida sana lakini yana uwezekano zaidi wa kutokea ikiwa:
Una hedhi ndefu zenye mtiririko mwingi sana wa damu
Hedhi yako sio ya kawaida (unakosa, inachelewa, au haitabiriki)
Wanawake wengine katika familia yako (kama mama yako) pia wana maumivu ya hedhi
Ulikuwa mdogo sana pindi ulipoanza hedhi yako (miaka 11 au mdogo zaidi)
Uko chini ya miaka 30
Ni mvuta sigara
Dalili za kabla ya hedhi (PMS) pia zinaweza kusababisha maumivu makali ya tumbo. Hata hivyo, maumivu ya dalili za kabla ya hedhi yaani PMS ni tofauti na maumivu ya kawaida ya hedhi. Kwa mfano, dalili za kabla ya hedhi yaani PMS zinaweza kusababisha uongezekaji uzito, tumbo kujaa, hali ya moyo ibadilikayo upesi, na kujihisi kuchoka. Utofauti mwingine ni kwamba maumivu ya kawaida ya hedhi mara nyingi huanza siku 1-2 kabla ya hedhi yako na hukaa kwa siku chache. Dalili za kabla ya hedhi yaani PMS huanza mapema zaidi, karibu wiki 1-2 kabla ya hedhi yako. Ikiwa unafikiri una dalili za kabla ya hedhi yaani PMS, muone mtaalamu wako wa afya kwa ajili ya njia za kutibu dalili zako.
Dondoo & Mbinu
Ingawa maumivu ya hedhi ni ya kawaida, ni machungu na yanayohisika vibaya. Hizi hapa ni mbinu baadhi za kiasilia za kutuliza maumivu yako:
Fanya mazoezi! Pindi unapofanya mazoezi, mwili wako hutoa endofini, ambazo ni vichocheo vya “furaha” ambavyo hutuliza maumivu na kuboresha hali yako ya moyo. Hivyo kwenda kwenye matembezi au kufanya yoga kunaweza kukusaidia ujihisi vizuri zaidi.

Jipe Joto! Joto linaweza kulegeza misuli katika mfuko wako wa uzazi. Kuweka chupa ya maji ya moto au taulo la moto chini ya tumbo lako kunaweza kulegeza misuli yako na kutuliza maumivu makali ya tumbo. Kuoga maji ya moto kunaweza pia kusaidia misuli yako kulegea.
Kunywa Maji Mengi! Kunywa maji ya vuguvugu au ya moto, kama chai, kunaweza kusaidia misuli yako kulegea na kuzuia ujaaji tumbo wenye maumivu.
Pata mapumziko mengi!
Epuka kutumia pombe na tumbaku!
Chaguo jingine kwa ajili ya kutuliza maumivu ni kutumia dawa, kama ibuprofen. Mtaalamu wako wa afya anaweza kupendekeza kutumia uzazi wa mpango wenye vichocheo (kama vidonge) kuweka sawa mzunguko wako na kutuliza maumivu yako ya tumbo.
Wakati gani wa kumuona daktari
Maumivu ya hedhi yenyewe hayapelekei matatizo mengine ya kiafya lakini yanaweza kufanya ikawa vigumu kufanya shughuli za kila siku kama kwenda shule au kazini. Hata hivyo maumivu ya hedhi yanaweza pia kusababishwa na magonjwa makubwa zaidi ya kiafya kama endometriosisi au vivimbe kwenye mayai.
Huu hapa ndio wakati gani unapaswa kumuona mtaalamu wa afya:
Maumivu yako ya hedhi yanakuzuia kufanya shughuli za kawaida (kama kwenda shule au kazini)
Una miaka zaidi ya 25 na unapata maumivu ya tumbo kwa mara ya kwanza
Una homa inayoambatana na maumivu yako ya hedhi
Una maumivu ya tumbo hata wakati haupo kwenye hedhi yako
Hizi ni ishara kwamba kitu fulani kingine kinasababisha maumivu yako. Kutibu sababu ndio njia nzuri zaidi ya kupunguza maumivu yako, hivyo mtembelee mtaalamu wako wa afya ikiwa lolote kati ya haya linatokea kwako.

Maumivu ya hedhi ambayo hayasababishwi na ugonjwa mwingine wa kiafya huwa na tabia ya kutulia kadri unavyokuwa na umri mkubwa zaidi au baada ya kujifungua. Hata hivyo maumivu ya mwanamke mara nyingi hupuuzwa na hutibiwa visivyo kikamilifu ukilinganisha na wanaume. Ndio maana ni muhimu kuusikiliza mwili wako, kuyaelezea mwenyewe mawazo na hisia zako, na kuongea na mtaalamu wako wa afya ikiwa una wasiwasi kwamba maumivu yako ya hedhi ni ishara ya kitu fulani kikubwa zaidi.
Una maswali kuhusu kujamiiana, maambukizi ya magonjwa ya zinaa yaani STIs, na uzazi wa mpango? Kumbuka unaweza kuchati na Nivi kwenye WhatsApp na Facebook Messenger muda wowote. Ni mazungumzo binafsi, ya usiri, na bure!
Commentaires