Kila Kitu Unachohitaji Kujua Kuhusu Kufanya Mapenzi kwa Njia ya Mdomo
Kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo ni aina ya tendo la kujamiiana ambalo linaweza kufanywa kwa kupitia kusisimuana kwa mdomo kati ya wapenzi. Linaweza kufanyika kutokana na sababu nyingi, aidha mnataka kunogesha uhusiano wenu, hamko tayari kujamiiana, au mnataka tu kujaribu kitu kipya! Hata hivyo, ingawa mapenzi kwa njia ya mdomo yanaweza kuwa tendo la kujamiiana linalosisimua kujaribu, kuna tahadhari pia za kuchukua. Endelea kusoma kujifunza kuhusu mapenzi kwa njia ya mdomo ni nini, dhana potofu zilizozoeleka, na jinsi ya kuwa salama ukiwa unafanya mapenzi kwa njia ya mdomo!
Mapenzi kwa Njia ya Mdomo ni Nini?
Mapenzi kwa njia ya mdomo ni tendo la kujamiiana ambalo unatumia mdomo wako, midomo, na/au ulimi kuzisisimua sehemu za siri za mtu mwingine. Inaweza kuhusisha, lakini isiishie kwenye kunyonya au kuramba uume, uke, njia ya uke, kisimi na/au mkundu. Inaweza kuhusisha muunganiko wowote wa wapenzi, aidha ni mwanaume akimsisimua mwanamke, mwanamke akimsisimua mwanamke, au mwanaume akimsisimua mwanaume au muunganiko wowote uliopo!
Dhana Potofu Zilizozoeleka Zinajibiwa
Mapenzi kwa Njia ya Mdomo yanaweza kusababisha ujauzito?
Hapana! – Haiwezekani kabisa kupata ujauzito kutokana na kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo, hata kama mbegu za kiume zikimezwa. Njia pekee ya kupata ujauzito kutoka kwenye mbegu za kiume au shahawa ni ikiwa zikiingia kwenye uke. Pindi mbegu za kiume zikimezwa, huingia tumboni na kamwe haziingiliani na viungo vya uke.
Ndio! – Pindi wanapojihusisha na kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo watu wengi huwa hata hawafikirii kuhusu ni nini majimaji ya kujamiiana yanaweza kuifanyia midomo yao. Hata hivyo, kama tu ambavyo ungesugua meno yako baada ya kula mlo, unapaswa kufanya hivi baada ya kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo, pia! Hii ni kwa sababu shahawa mara nyingi zina asili ya asidi na zinaweza kudhuru meno yako kama hautayasugua baada ya kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo.
Ninaweza kupata STI kwa kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo?
Ndio! – Kinyume na imani maarufu maambukizi mengi ya magonjwa ya zinaa yaani STI yanaweza kuambukizwa kwa kupitia kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo. Kwa mfano, mkanda wa jeshi unaweza kuambukizwa kutokana na kugusana kwa ngozi na ngozi ambako hutokea wakati wa kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo. Magonjwa mengine ya zinaa yaani STI yanaweza kuliambukiza koo lako kutokana na kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo kama kisonono na klamidia, na magonjwa makubwa zaidi ya zinaa ambayo unaweza kuambukizwa ni kaswende, homa ya ini B na HPV.
Hapana! – Aidha ni kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo au kujamiiana kwa njia ya kawaida, maambukizi yatasambaa kama ulinzi wa kizuizi hautatumika. Hii inamaanisha, kondomu au kikinga kinywa lazima kitumike ili kulinda dhidi ya kusambaa kwa ugonjwa. Aina yoyote ya kusuuza mdomo, aidha ni pombe, sabuni na maji, au kingine chochote kile kinachofikiriwa hakitalinda dhidi ya STI.
Je! Ninatakiwa kuhusisha ngono salama katika kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo?
Ndio! – Mara zote ni muhimu kufanya ngono salama pindi unapojihusisha na kufanya mapenzi, ikihusisha kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo. Endelea kusoma kufahamu njia za kubakia salama wakati ukifanya mapenzi kwa njia ya mdomo!
Jinsi ya Kufanya Mapenzi Salama kwa Njia ya Mdomo
Njia nzuri zaidi ya kufanya mapenzi salama kwa njia ya mdomo ni kwa mnyonywaji kuvaa kikinga mdomo au kondomu. Huu ni ulinzi mzuri zaidi kwasababu huwa kama kizuizi dhidi ya maambukizi yoyote yanayoweza kutokea na mdomo wako. Njia nyingine za kupunguza hatari ya STI ni kuepuka kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo ikiwa wewe au mtu mwingine ana STI, ana mikatiko au vidonda ndani ya mdomo wake au sehemu zake za siri au ikiwa anayenyonya ana maambukizi ya koo. Hizi zote ni ishara ambazo huongeza uwezekano wa kusambaa kwa STI, hivyo ni muhimu kuepuka hali zinazohusisha hatari hizi.
Kwa ujumla, kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo ni shughuli ifurahishayo kuyabadilisha maisha yako ya kimapenzi, lakini bado uhitaji ulinzi na ridhaa. Aidha ni kunogesha maisha yako ya kimapenzi, kujaribu kitu fulani kipya, au unapendelea kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo, kumbuka kutumia njia ya kizuizi kuepuka kuambukizwa STI yoyote. Ili mradi wapenzi wote wawili mko pamoja katika hilo, furahieni na stareheni!
Unataka kujifunza zaidi? Una maswali mengine kuhusu kujamiiana, maambukizi ya magonjwa ya zinaa yaani STIs, UKIMWI, au uzazi wa mpango? Kumbuka unaweza kuchati na Nivi kwenye WhatsApp na Facebook Messenger muda wowote. Ni mazungumzo binafsi, ya usiri, na bure!
Comentarios