Kifua Kikuu: Ni nini, Kwanini ni muhimu, na Jinsi ya Kupata Vipimo na Matibabu
Kisia nini? Leo ni Siku ya Kifua Kikuu Duniani! Na kama siku zote za [insert disease here] duniani, dhumuni lake ni kukuza ufahamu ili kwamba watu wengi zaidi wafahamu ni wakati gani, na jinsi gani, ya kutafuta msaada kwa ajili yao na wapendwa wao. Kwasababu maarifa huokoa maisha! Hivyo, hebu tujitayarishe na tuingie kazini: Kifua Kikuu ni nini, na kwanini ni muhimu?
Kifua Kikuu ni nini?
Kifua Kikuu—au TB kwa kifupi—ni maambukizi ya mapafu yanayosababishwa na bakteria (hasa Myobacterium tuberculosis). Na ni ya kawaida sana! Kawaida sana, kiukweli, kwamba 25% ya watu duniani wana TB muda huu. Hao ni watu wengi sana!
Unaweza ukashangaa hilo linawezekanaje—ikiwa watu wengi sana wanatembea wakiwa wagonjwa wa TB, kwanini hatuisikii zaidi? Vizuri, kuna jibu rahisi kwa hilo: watu wengi mbalimbali wenye TB hawajui wanayo. Kwasababu miili yetu iko vizuri sana katika kupigana na magonjwa, watu wengi wenye TB hawana dalili kabisa (ikimaanisha hawapati dalili zozote). Bakteria “hulala” tu katika mapafu kwa miezi au miaka mingi mpaka mfumo wako wa ulinzi wa mwili (mfumo wa kinga) unapodhoofishwa na kitu kingine—kama kuumia, saratani, au ugonjwa au maambukizi mengine. Hiyo ndio fursa yake kushambulia. Pindi mtu anapokuwa hatarini kupata maambukizi, bakteria wa TB watakua na kuzaliana; wakisababisha dalili, ugonjwa mkali na hata kifo.
Hii ndio sababu kubwa kwanini TB ni suala la muhimu hivyo—kwasababu watu wenye mifumo dhaifu ya kinga hawawezi kujilinda wenyewe dhidi ya magonjwa makali, ni tatizo kubwa kwamba TB pia ipo sana. Tabia na hali nyingi hudhoofisha mfumo wa kinga wa mwili, pia; na hizo pia humfanya mtu kuwa na uwezekano zaidi wa kupata dalili kali za TB. Hii hapa ni baadhi ya mifano:
UKIMWI
Kisukari
Utumiaji/Utumiaji mbaya wa dawa za kulevya
Kuvuta sigara
Kunywa pombe
Kufanya kazi mazingira yenye hatari kubwa (kama kituo cha afya, nyumba ya uuguzi, makazi ya wasio na makazi, gerezani, au mgodini)
Kumbuka: tabia, hali, na mitindo hii ya maisha haisababishi TB—inamfanya tu mtu kuwa hatarini zaidi kupata dalili kali. Unaweza tu kupata TB kwa kuvuta hewa yenye vijidudu ya mtu mwenye kifua kikuu.
Dalili za TB ni zipi?
Dalili za TB ni sawa na dalili za maambukizi mengine ya mapafu na upumuaji, kama mafua au UVIKO-19. Hizi hapa ni dalili zilizozoeleka:
Homa
Kupoteza uzito
Kutokwa jasho usiku
Kikohozi endelevu (kikohozi ulichokuwa nacho kwa wiki nyingi)
Lakini kumbuka: watu wengi wenye TB hawana dalili, na hivyo hawatapata dalili yoyote kati ya hizo za juu. Ndio maana kupima TB ni muhimu sana—mara nyingi ndio njia pekee unayoweza kufahamu ikiwa una TB, na ndio njia pekee ya kuitofautisha na aina nyingine za maambukizi sawia.
Ninaweza vipi kuzuia TB?
Vitu vingi vya kutisha vimesababishwa na janga la UVIKO-19, lakini kitu kimoja kizuri ni kwamba kila mmoja duniani ana ufahamu zaidi juu ya vijidudu, hali ya usafi, na kuepuka maambukizi. Na kwa bahati nzuri, mengi kati ya mazoea na tabia tulizozizoea wakati wa janga la UVIKO-19 zinaweza kutusaidia kuepuka TB, pia; na pia kuepusha kuisambaza kwa wengine.
Vitu kama:
Kuvaa barakoa ukiwa kwenye makundi makubwa ya watu
Kuepuka mikusanyiko (ukiwa unachangamana, weka umbali kati yako na wengine)
Kufunika pua na mdomo wako pindi ukikohoa au kupiga chafya
Kuosha mikono yako mara kwa mara
Kutupa mbali tishu zozote baada ya kuzitumia
Kufungua milango na madirisha mara kwa mara (hii husaidia hewa kupita katika nyumba yako, kitu ambacho kinaweza kusaidia magonjwa ya upumuaji yasisambae kutoka kwa mtu hadi mtu)
Ninaweza kufahamu vipi kama nina Kifua Kikuu, na kinatibiwaje?
Aina ya kipimo cha TB kilichozoeleka sana ni kile kinachoitwa “kipimo cha makohozi.” Kwa kipimo cha makohozi, mtaalamu wa huduma za afya atakuomba ukohoe na atakusanya mate au makohozi yoyote mazito ambayo yatatoka mdomoni mwako. Halafu, atayapima TB (eksirei za kifua pia ni njia iliozoeleka ya kuchunguza TB).
Na kama TB ilivyo hatari, kiukweli inatibika kabisa! Mara nyingi, matibabu uhusisha kutumia antibayotiki moja au zaidi kila siku kwa kipindi cha miezi michache. Sehemu “ngumu” pekee kuhusu matibabu ya TB ni kwamba unatakiwa kukumbuka kutumia dawa zako kila siku—kama ukifanya makosa kizembe au ukisahau mara kwa mara, mwili wako unaweza usiwe na uwezo wa kuwaondoa bakteria wote wa TB; kitu kinachomaanisha wanaweza kuendelea kukua na kukufanya uwe mgonjwa, baadae.
Ni kweli kwamba TB inaweza kuwa ya kutisha, na kwa hakika ni suala muhimu sana, duniani kote. Lakini kwa heshima ya Siku ya TB Duniani, sisi hapa Nivi tuna habari njema kwa ajili yako: Upimaji na matibabu ya TB kiukweli ni rahisi sana sio tu kwasababu yanapatikana katika maeneo mengi na ni yasio na maumivu kabisa, lakini pia kwasababu, kupitia askNivi, una ufikiaji binafsi wa huduma za upimaji na matibabu ya TB katika eneo lako, BURE, moja kwa moja kupitia simu yako, kompyuta, au tableti! Bofya tu kwenye moja kati ya viunga hapo chini kuanza mazungumzo na Nivi kwenye WhatsApp au Facebook Messenger—Nivi inaweza kupendekeza huduma kulingana na eneo lako, na haitashirikisha yoyote kati ya taarifa zako na washirika wengine. Ni huduma ya afya, imefanywa rahisi.
Unataka kutafuta sehemu upate kipimo cha TB au matibabu ya TB? Au labda unataka tu kujifunza zaidi kuhusu TB? askNivi ina taarifa nyingi sana juu ya TB na maada nyingine za afya. Chati na Nivi kwenye WhatsApp au Facebook Messenger muda wowote na uunganishwe kwenye taarifa na huduma za afya unazohitaji. Ni ya kibinafsi, ya usiri, na bure!
Comments