top of page

Chanjo ya UVIKO-19: Jitihada yetu kubwa kwenye kupambana na janga hili kubwaPamoja na kuvaa barakoa na kuepuka misongamano, uchomaji chanjo ni njia fanisi ya kujilinda dhidi ya Uviko-19 na kupunguza hatari ya kusambaza virusi hivyo. Serikali ya Kenya imelenga kutoa chanjo kikamilifu kwa watu wazima wote waishio Kenya ifikapo Juni 2022. Hadi kufikia Januari 22 mwaka huu 2022, Wizara ya Afya ya Kenya (MOH) imeripoti zaidi ya watu wazima milioni 23 waliochoma chanjo, kati yao milioni 5, au 18.6% ya jumla ya idadi ya watu wazima, wamepata chanjo kwa ukamilifu. Endelea kusoma ili maswali yako kuhusu chanjo yajibiwe!


Je! Ni chanjo zipi za UVIKO-19 zinazopatikana Kenya

Pindi chanjo inapoonekana kuwa salama na fanisi, inaidhinishwa na mamlaka za udhibiti za kitaifa na kusambazwa kwa watu. Wizara ya Afya ya Kenya imeidhinisha matumizi ya chanjo za Covishield, Pfizer, Moderna, Sinopharm, na Johnson & Johnson. Chanjo za AstraZeneca/Covishield, Pfizer, Moderna na Sinopharm zinahitaji dozi mbili ili mtu awe amepata chanjo kwa ukamilifu, hivyo unapaswa kupanga kupata dozi yako ya pili wiki 4-12 baada ya dozi ya kwanza. Dozi moja ya chanjo ya Johnson & Johnson hutoa ulinzi kamili. Chanjo zote za UVIKO-19 zilizoidhinishwa na kupendekezwa ni salama na fanisi kama ukipata dozi zote zilizopendekezwa.


Je! Ni wapi ninaweza kupata chanjo ya UVIKO-19?

Chanjo za UVIKO-19 zinapatikana bure bila malipo kwa watu wote waishio Kenya, ikihusisha wakimbizi na wahamiaji kuhakikisha upatikanaji wa sawa na kwa usawa. Unaweza kupata orodha iliyosasishwa ya vituo vilivyoandaliwa na kuidhinishwa vya utoaji chanjo hapa au piga namba ya simu ya Wizara ya Afya maalum kwa ajili ya UVIKO-19 kwenye 719.


Je! Ninaweza kupata vipi rekodi yangu ya uchomaji chanjo?

Programu ya uchomaji chanjo ya Kenya inasimamiwa kupitia hili Jukwaa, mfumo kamili ambapo unaweza kujipangia ratiba ya uchomaji wako wa chanjo ya UVIKO-19 na kupata cheti chako cha chanjo ya UVIKO-19. Unaweza kujifunza zaidi kwa kutazama hii video ya mafunzo juu ya jinsi ya kupata huduma hizi kupitia jukwaa hili la mtandaoni.


Tuchome chanjo!

Chanjo ni njia bora ya kukulinda wewe na jamii yako dhidi ya UVIKO-19 kupunguza hatari yako ya maambukizi au ukali wa dalili zako. Kadri watu wengi wanavyochoma chanjo, ndivyo tunavyoweza kuzuia kusambaa kwa UVIKO-19 zaidi na kuzuia kutokea kwa aina mpya za virusi. Kwa taarifa zaidi juu ya kupata kliniki karibu yako na kujisajili kwa ajili ya uchomaji chanjo, tafadhali tembelea https://www.health.go.ke.

 

Unataka kujifunza zaidi? Una maswali kuhusu kujamiiana, STIs, HIV/AIDS, au uzazi wa mpango? Kumbuka unaweza kuchati na Nivi kwenye WhatsApp na Facebook Messenger muda wowote. Ni kwa faragha, kwa usiri, na bure!留言


bottom of page