top of page
Website Banner v2 (1).jpg

Taarifa za bure, za faragha kuhusu vidhibiti mimba, magonjwa ya zinaa na mengine

Habari, mimi ni Nivi...

Mimi ni chatbot niko hapa kukupa ukweli kuhusu vidhibiti mimba, kujilinda dhidi ya magonjwa ya zinaa na mada nyinginezo za afya ya ngono na uzazi.

Ninaweza kukusaidia kupanga na kudhibiti maisha yako ya usoni. Unaweza kupiga gumzo nami 24/7. Ni bure, salama, ya faragha na ya siri.

 

Unapobonyeza kitufe cha waridi, neno hupakia kiotomatiki kwenye WhatsApp. Bonyeza kitufe la kutuma ili kuanza kuzungumza kuhusu afya yako!

askNivi inafanya kazi kwa hatua 3 rahisi:

Hatua ya 1

Bonyeza kitufe cha waridi ili kuanza kupiga gumzo. WhatsApp yako itafungua kiotomatiki na utaona neno kwenye kisanduku cha maandishi. 

Hatua ya 2

Tuma neno hili kwa kubonyeza kitufe cha kutuma. 

Hatua ya 3

Nitakuuliza maswali machache, tafadhali yajibu ili niweze kukufahamu zaidi kidogo. Kisha tunaweza kuchunguza mada za afya ya ngono!

Ukweli, sio Hadithi

Nivi ni kama shangazi yako mzuri ambaye ana majibu yote na hakuhukumu. Nivi anakupa ukweli ili uweze kuamua ni nini kinachokufaa

Mapendekezo ya Kibinafsi

Mwambie Nivi umri wako, jinsia na mahali unapoishi ili kupata mapendekezo ya kibinafsi. Nivi inaweza kukusaidia kupata mbinu ya kupanga uzazi inaofaa kwa mwili wako.

Pata Kliniki

Ni muhimu sana kuwa na kliniki nzuri. Nivi inaweza kukusaidia kupata eneo iliyo karibu nawe ili uweze kupata mbinu ya kupanga uzazi iliyo salama na ya kibinafsi wakati unahitaji.

Nivi ni Bure, Salama na ya Kibinafsi

Ni rahisi kuzungumza. Nivi inapatikana 24/7.

bottom of page